Ligi Kuu

Yanga yafunguka ishu ya Guede

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga imejibu maswali ya mashabiki wa timu hiyo juu ya hatma ya mshambuliaji Joseph Guede kuwa ipo kwenye mikono ya Kocha Miguel Gamond.

Guede alosajiliwa kipindi cha dirisha dogo kwa mkataba wa miezi sita ambao umetamatika baada ya kumalizika kwa msimu wa 2023/24.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa mshambuliaji huyo amemaliza mkataba wake ndani ya Yanga.

Amesema viongozi wapo makini katika suala la kufanya usajili na kila kitu kitawekwa wazi kuanzia Julai Mosi, 2024.

“Tunafahamu Wananchi wanatamani kujua hatma ya mshambuliaji wetu huyo ambaye amemaliza mkataba atasalia au anaondoka, majibu ya hayo yatapatikana Jumatatu, tutaweka wazi wanaosalia na wanaondoka,” amesema Kamwe.

“Kila Mwanayanga anatambua ubora wa mshambuliaji huyo na suala lake lipo mezani, kilichokuwepo sasa hivi ni kuboresha timu kulingana na mapungufu yalijitokeza msimu uliopita,” amesema Kamwe.

Related Articles

Back to top button