Nandy azindua tamasha lake
DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo fleva nchini, Faustina Mfinanga ‘Nandy’ amezindua rasmi Tamasha la Nandy Festival litakayozunguka mikoa yote nchini na kupambwa na wasanii tofauti tofauti.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akizindua tamasha hilo Nandy amesema wasanii watakaoshiriki wamejipanga kutoa burudani ya uhakika katika majukwaa mbalimbali watakayopanda.
“Baada ya mengi yaliyotokea, kulea na pilika za familia Mume wangu Billnass ameniruhusu ameniambia kuwa pamoja na ulezi anataka niendelee na kazi zangu kama kawaida.
“Niwaombe wasanii wawe tayari na mashabiki tunapokuja mikoani kwenu mtupokee na kufika uwanjani tutakapokuwa tunaburudisha, orodha ya wasanii ni wengi na tutahakikisha tunawataja hivi karibuni.”amesema Nandy
Pia ameongeza kuwa wasanii wakike watapewa kipaumbele katika kila mkoa watakao kwenda kutoa burudani huku kauli mbinu ya Nandy Festival ikiwa ‘Tupishee kila Mkoa’.