Kwingineko

Dortmund kulipiza kisasi vs PSG leo?

TIMU nane za mwisho kufuzu hatua ya 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya zitajulikana leo baada ya michezo nane kupigwa viwanja tofauti.

Mchezo kivutio utazikutanisha Borussia Dortmund itakayoikaribisha Paris Saint-German katika kundi F kwenye uwanja wa Signal Iduna Park, jijini Dortmund.

Katika mchezo wa kwanza Septembe 19, 2023, PSG iliichapa Dortmund kwa mabao 2-0.

Michezo mingine ni kama ifuatavyo:

KUNDI E
Atletico Madrid vs Lazio
Celtic vs Feyenoord

KUNDI F
Newcastle United vs AC Milan

KUNDI G
FK Crvena Zvezda vs Manchester City
RB Leipzig vs Young Boys

KUNDI H
FC Porto vs Shakhtar Donetsk
Royal Antwerp vs Barcelona

Timu zilizokwishafuzu hatua ya 16 bora ni Bayern Munich, FC Copenhagen, Arsenal, PSV Eindhoven, Real Madrid, Napoli, Real Sociedad na Inter Milan.

Related Articles

Back to top button