Muziki

Dola milioni 71 zamstaafisha rapa T.I. kwenye maonesho ya LIVE

NEW YORK: RAPA wa Marekani Clifford Harris Jr maarufu T.I amesema hatotumbuiza tena katika maonesho ya ‘LIVE’ baada ya kumaliza tamasha lake la Desemba 19 litakalo fanyika Atlanta nchini humo.

Rapa huyo mwenye miaka 44 amesema baada ya onesho la 93.1 aliloliita ‘The Beat’s Jingle Ball’ hatotumbuiza tena kwa sababu hatokuwa akitafuta tena pesa kupitia matamasha, wala mialiko mbalimbali ya kumuonesha msanii huyo.

Kwenye kipindi cha 96.1 cha ‘Rari at 2’ cha The Beat, alisema: “Nawashukuru nyote kwa kunipa tamasha la mwisho la kufanya kazi, kwa sababu sihitaji pesa tena. Sitaki kuifanya tena. … Sitaki watu wanilipe ili kuruka ruka na kutoa jasho kwa burudani yao.”

Onesho la 93.1 la The Beat’s Jingle Ball pia litajumuisha maonyesho kutoka kwa Tinashe, Sexyy Red, T-Pain, Saweetie, Khalid na The Kid LAROI.

Sababu kuu inayodaiwa kumfanya T.I. kutotaka tena pesa za show za matamasha ni kwa sababu yeye na mke wake Tiny hivi majuzi walishinda kesi na walilipwa fidia ya dola milioni 71.

T.I na mkewe Tiny walishinda kesi dhidi ya kampuni ya MGA Entertainment, ambao walikiuka haki miliki ya kikundi chao cha muziki cha OMG Girlz na kampuni yao ya L.O.L. Amazing! O.M.G. dolls.

Related Articles

Back to top button