
LIGI kuu ya soka Tanzania Bara inarejea leo baada ya kupisha ratiba ya kimataifa kwa michezo mwili kupigwa Dar es Salaam na Singida.
Dodoma Jiji ambayo imetoka sare michezo miwili na kupoteza miwili ikishika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 2 itakuwa mwenyeji wa Geita Gold kwenye uwanja wa Liti mjini Singida.
Geita Gold ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 3 baada ya michezo 4.
Wagosi wa kaya, Coastal Union kutoka Tanga itakuwa mgeni wa wajeshi Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Ruvu Shooting inashika nafasi ya 7 ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 4 wakati Coastal Union ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 4 baada ya michezo 4 pia.