Nyumbani

Dk Nchemba ampa tano Bakhresa kwa uwekezaji

DODOMA: WAZIRI wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amempongeza Said Salim Bakhresa kwa uwekezaji mkubwa katika tasnia ya michezo ambao umekuwa chachu ya maendeleo ya michezo nchini, hususan kupitia
matangazo ya moja kwa moja (mubashara).

Akizungumza Bungeni jijini Dodoma jana Dk Nchemba amesema: “ni ukweli usiopingika kuwa, maisha ya watu hayawezi kukamilika kama hayana furaha, hilo tumeliona kupitia Azam TV ambayo si tu wamefanya kila mtu kuzungumzia mpira wa miguu wa nchi hii,

“lakini pia wameinua maisha ya wachezaji hasa wa ngumi, mpira wa miguu pamoja na wacheza filamu kupitia tamthilia mbalimbali za kitanzania,”

Amesema licha ya kuwa kampuni hii ni ya binafsi, lakini sasa imekuwa kama mali ya umma kutokana na umuhimu wake katika jamii ya Tanzania.
Mwisho

Related Articles

Back to top button