Ligi KuuNyumbani

Prisons yaiweka korokoroni Simba

IKITOKA kuifunga Jwaneng Galaxy ya Botswana mabao 6-0 mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, klabu ya Simba leo imeonja joto ya jiwe baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mchezo huo umefanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambako Simba imehamishia michezo yake ya ndani baada ya viwanja vya Benjamin Mkapa na Uhuru, Dar es Salaam kuwa katika matengenezo.
Katika dabi ya kijeshi Mashujaa imeutumia vema uwanja wa nyumbani wa Lake Tanganyika mjini Kigoma baada ya kuifunga JKT Tanzania  bao 1-0.
                          FULLTIME
SIMBA                 1 – 2      TZ PRISONS
Fabrice Ngoma 89′             Samson Mbangula 45+3′, 62′
MASHUJAA           1 – 0      JKT TANZANIA
Mapinduzi Balama 7′

Related Articles

Back to top button