Mastaa
D Voice afichua mahusiano yake na Lulu Diva

DAR ES SALAAM:MSANII wa Bongo fleva kutoka lebo ya Wasafi, D Voice ameweka bayana mahusiano yake ya kimapenzi na msanii mwenzake Lulu Abas ‘Lulu Diva’.
D Voice amesema kuwa mahusiano hayo wameyaficha kwa muda mrefu lakini kwa sasa hakuna Siri tena kwank wameamua kuyaweka hadharani.
“Lulu Diva ni mpenzi wangu lakini hatuishi pamoja kwa kuwa bado hatujafanya taratibu zinazotakiwa kufuatwa. Tukikamilisha,tutaishi pamoja lakini kwa sasa naishi na kaka yangu”,amesema D Voice.
Akaongeza kwa kusema “Nipo nae kwenye mahusiano na tuna malengo ya kufika mbali. Nimeona watu wakiuliza mara nyingi na sasa hakuna haja ya kuficha tena, wajue tu sisi ni wapenzi”.