Mastaa

Demu wa Facebook awajengea nyumba wazazi wake

NAIROBI: MTAYARISHAJI wa maudhui ya vichekesho nchini Kenya maarufu kwa jina la Demu Wa Facebook ameonyesha nyumba ya vyuma vitatu anayowajengea wazazi wake kutokana na kipato cha sanaa anayofanya.

Msichana huyo maarufu nchini Kenya na wafuatiliaji wa sanaa ya Kenya ameweka video katika channeli yake ya YouTube akionekana akiendelea na ujenzi wa nyumba hiyo, akionyesha shukrani kwa Mungu kwa hatua ambayo amefikia.

Pia aliwashukuru wanawake wote wanaompa pongezi kutokana na ujenzi huo wakiamini kwamba mwanamke huyo mchekeshaji amefanya jambo kubwa kwa Maisha yake kwa namna alivyopambania sanaa yake.

“Mambo ya mungu na bidii, nimeamua kujenga wazazi wangu nyumba ili wakae vizuri wakiwa bado hai. Wanawake wengi wamenipongeza na kuniunga mkono katika hatua hii Mungu awabariki kwa maana wamenitia nguvu ya kukamilisha nyumba hii ndiyo maana nimeamua niwaonyeshe hatua ya ujenzi wa nyumba hii ulipofikia,” ameeleza Demu wa facebook.

Dem Wa Facebook alieleza kwamba alichagua kuwajengea wazazi wake nyumba hiyo si kwa sababu ya upendo tu bali pia kwa sababu yeye ndiye mlezi wa familia na anataka kuwa mfano mzuri kwa wasanii na vijana wengine wafanye hivyo kwa wazazi wao.

“Hii nyumba nimejenga miezi mitatu sasa imefikia hapa natumaini hadi December itakamilika ili tuifungue wazazi waanze kuishi kwenye nyumba yao bora mimi ndiyo mlezi wa hawa wazazi lazima niwatunze hivi vijana wengine muige mfano wangu,” alieleza.

Related Articles

Back to top button