Chelsea yakomba tuzo za Septemba
LONDON: Meneja wa Chelsea Enzo Maresca na mshambuliaji wa klabu hiyo Cole Palmer wameng’aa katika tuzo za mwezi za ligi kuu ya England baada ya wawili hao kutwaa tuzo ya meneja wa mwezi na mchezaji bora wa mwezi
Palmer alieanza ligi kwa kishindo anatwaa tuzo ya pili ya mchezaji bora wa mwezi katika maisha yake ya ligi hiyo pendwa Duniani baada ya ile ya mwezi Aprili mwaka huu akifunga mabao 5 ikiwemo hat-trick moja ndani ya mwezi Septemba.
Maresca kwa upande wake amewaongoza vigogo hao wa magharibi mwa London katika michezo mitano ndani ya mwezi Septemba akishinda minne na sare mmoja.
Chelsea wamekuwa na msimu bora mpaka sasa wakiwa nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi 14. Wamecheza mechi 7 wakishinda 4, sare 2 na kupoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Manchester City.