EPL

Gwiji KDB sasa mechi 400 Man City

MANCHESTER: SASA ni rasmi ‘staa’ wa Manchester City Kevin De Bruyne atacheza mchezo wake wa 400 tangu awasili klabuni hapo kutokea Bundesliga kunako klabu ya Wolfsburg Agosti 2015.

KDB ameifungia Manchester City mabao 104 katika michezo 399 ya awali. Msimu huu Amecheza dakika 734 katika michezo 12 pekee, nane kati ya hiyo akianza katika kikosi cha kwanza na tayari amehusika na mabao manne (magoli 2, asisti 2).

Kabla ya kuwasili Etihad, De Bruyne amecheza michezo 339 katika klabu mbalimbali ikiwemo Chelsea, Werder Bremen, na Genk ya nyumbani kwao Ubelgiji pamoja na timu za taifa ile ya wakubwa na za vijana wa U19 na U21 ambako kote amefunga mabao 182.

Hii inamfanya kiungo huyo kufikisha jumla ya michezo 735, ‘asisti’ 304 na magoli 181 maisha yake ya soka kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button