Nyumbani

Charles M’Mombwa atua Zabbar St. Patrick

VALLETA: KIUNGO wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles M’Mombwa amekamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya Zabbar St. Patrick FC ya Malta.

Kupitia taarifa rasmi ya klabu hiyo, Zabbar St. Patrick imeeleza kufurahishwa na ujio wa M’Mombwa mwenye umri wa miaka 28, ambaye anajiunga na timu hiyo baada ya kuwa na msimu bora akiwa na Floriana FC.

Msimu uliopita, M’Mombwa alikuwa miongoni mwa wachezaji muhimu walioisaidia Floriana kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Malta, akionesha kiwango bora katika eneo la kiungo.

Zabbar St. Patrick imesema kiungo huyo ana sifa za kupambana, ubora wa kiufundi, uzoefu na uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii uwanjani, mambo ambayo yanatarajiwa kuongeza nguvu katika kikosi chao kuelekea msimu mpya.

Mbali na mafanikio yake katika ngazi ya klabu, M’Mombwa ni mchezaji wa mara kwa mara wa Taifa Stars, jambo linalothibitisha kiwango na uzoefu wake katika soka la kimataifa.

Ujio wa nyota huyo wa Tanzania unatajwa kuwa sehemu ya maboresho ya kikosi cha Zabbar St. Patrick kinachojiandaa kwa changamoto za msimu ujao wa mashindano nchini Malta.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button