Casemiro kutimkia Saudi Arabia

TETESI za usajili zinasema kiungo wa Manchester United, Carlos Henrique Casimiro maarufu Casemiro anaweza kuondoka klabu hiyo majira haya ya kiangazi kufuatia nia ya vilabu vya ligi ya kulipwa Saudi Arabia vya Al Nassr, Al Ahli na Al Qasidiya kuhistaji huduma yake.((GOAL – Brazil)
Ripoti nyingine zinasema West Ham inakaribia kufikia dili la pauni mil 15 kumnasa beki huyo wa Brazil.(Guardian)
Chelsea ni mingoni wa vilabu kadhaa vya Ligi Kuu England vinavyoonesha nia kumsajili winga wa Leeds United, Crysencio Summerville.
Pia Liverpool imehusishwa na mchezaji huyo wa kidachi. (Daily Telegraph)
Klabu ya Barcelona inasemekana kutia mguu katika klabu ya Atalanta kuona uwezekano wa kumsajili Éderson José dos Santos Lourenço da Silva, ‘Éderson’, ambaye pia anafuatiliwa na Liverpool na Tottenham Hotspur. (Calciomercato – Italy)
Fowadi wa England wa klabu ya Manchester United Mason Greenwood, 22, anataka kurejea timu ya Getafe ya Hispania msimu ujao baada ya kucheza mechi ya mwisho akiwa kwa mkopo katika timu hiyo ya La Liga. (Teamtalk), external
Wanafainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Borussia Dortmund inavutiwa kumsajili Greenwood, ambaye kwa mara ya mwisho alivaa uzi wa Manchester United Januari, 2022. (ESPN)
West Ham imekubaliana na klabu ya Flamingo dili la pauni mil 15m kumnunua beki wa Brazil,28, Fabricio Bruno. (Guardian)
Aston Villa na Crystal Palace zinaangalia uwezekano wa uhamisho wa beki wa klabu ya Gent, Archie Brown, 22. (Mirror)
Barcelona inaweza kujaribu kumrejesha fowadi mreno Joao Felix,24, toka Atletico Madrid kwa kipindi cha pili baada kucheza kwa mkopo Nou Camp msimu uliopita. (Sport – in Spanish)