Tottenham yamtupia macho Conor Gallagher
TETESI za usajili zinasema Tottenham itatuma ofa ya kumsajili kiungo wa Chelsea Conor Gallagher majira yajayo ya kiangazi iwapo kiungo huyo wa England, 24, atashindwa kufikia makubaliano ya kongeza mkataba wake unaofikia tamati mwisho wa msimu ujao (Telegraph – subscription required)
Newcastle United na Arsenal zipo katika tahadhari baada ya mazungumzo kati ya Brentford na mshambuliaji wa England, 27, Ivan Toney kukwama. (TeamTalk)
Brentford ina nia kumsajili mshambuliaji wa Lille raia wa Canada, Jonathan David, 24, kuwa mbadala iwapo Toney ataondoka klabu hiyo majira ya kiangazi. (Football Transfers)
Manchester United na Tottenham zipo katika juhudi kusaka saini ya Jarrad Branthwaite wa Everton wakati Chelsea, Arsenal na Real Madrid zimeonesha nia kumsajili beki huyo wa kati wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21.(Mail)
Newcastle imeungana na West Ham katika mbio za kusamjili fowadi wa Genoa, raia wa Iceland, Albert Gudmundsson, 26. (Gazzetta dello Sport – in Italian)
Arsenal inaishiwa uvumilivu dhidi ya kiungo mjerumani wa klabu hiyo Kai Havertz na inafikiria kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 majira ya kiangazi. (Fichajes – in Spanish)