Tetesi

Tetesi za usajili

KATIKA kinachofikiriwa kuwa pigo kwa Real Madrid, mazungumzo ya awali yanafanyika kati ya Kylian Mbappe na Paris Saint-Germain kuhusu kuongoza mktaba ingawa itahusisha kipengele cha kuachiwa 2014. (Fabrizio Romano)

Liverpool bado inaweza kuwa kituo mbadala kwa Kylian Mbappe, ambaye anamhusudu Jurgen Klopp na anaweza kushawishika iwapo The Reds itatoa ofa.(L’Equipe)

Al Ittihad inaamini Mohamed Salah anataka kujiunga na klabu hiyo wakati mazungumzo na Liverpool yakiendelea. Kocha wa The Reds Jurgen Klopp anasisitiza hataki kumpoteza nyota huyo wa Liverpool.(90min)

Chama cha Soka England(FA) kinasemekana kuwa na nia ya kumwaajiri kocha wa Manchester City Pep Guardiola kuwa kocha ajaye wa England mara Gareth Southgate atakapoachia ngazi.(Mirror)

Chelsea inafikiria kumwania mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney Januari, 2024.

Kiungo wa Real Sociedad, Martin Zubimendi kwa muda mrefu amehusishwa kujiunga na Barcelona lakini Arsenal inaweza kumnunua nyota huyo anayechipukia mwezi Januari, 2024.

Related Articles

Back to top button