Mastaa

Brooklyn Beckham afichua siri ya mgogoro wa wazazi wake

LONDON: BROOKLYN Beckham, mtoto mkubwa wa nyota wa zamani wa soka David Beckham na mbunifu wa mitindo Victoria Beckham, amezua gumzo kubwa duniani baada ya kuzungumza kwa mara ya kwanza taarifa za kuwepo kwa mgogoro ndani ya familia yake.

Brooklyn, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na taarifa za kutofautiana na baadhi ya wanafamilia wake, alitoa kauli iliyowafanya mashabiki na vyombo vya habari kuanza kujadili upya hali halisi ya mahusiano ndani ya familia hiyo maarufu duniani.

Katika ujumbe uliovutia hisia za wengi, Brooklyn alidokeza kuwa mambo ndani ya familia yake si rahisi kama yanavyoonekana kwa nje, akisisitiza kuwa wakati mwingine familia hukumbana na changamoto ambazo haziwezi kueleweka kwa urahisi na watu wa nje.

Kauli hiyo imekuja baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuhusu kuwepo kwa mvutano kati yake na baadhi ya ndugu zake pamoja na watu wa karibu wa familia ya Beckham.

Hata hivyo, Brooklyn hakutoa maelezo ya kina kuhusu chanzo cha tofauti hizo wala hakumtaja mtu yeyote chanzo cha mgogoro huo.

Mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wameonesha hisia tofauti kuhusu kauli hiyo. Wapo waliomsifu kwa kuamua kuzungumza hadharani kuhusu hali inayomkabili, huku wengine wakitaka familia hiyo kutafuta suluhu ya tofauti zao kwa faragha.

Familia ya Beckham imekuwa miongoni mwa familia zinazofuatiliwa zaidi duniani kwa zaidi ya miongo miwili, kutokana na mafanikio makubwa ya David Beckham katika soka na ushawishi mkubwa wa Victoria Beckham katika tasnia ya mitindo na burudani.

Hadi sasa, hakuna tamko rasmi lililotolewa na David Beckham au Victoria Beckham kujibu kauli za mtoto wao huyo kila mmoja ameonekana akiwa bizi na kazi zake.

Related Articles

Back to top button