Mastaa

Billnas wala hana shida kufanya kazi na Mkewe

DAR ES SALAAM: Msanii wa muziki wa kizazi kipya Faustina Mfinanga ‘Nandy’, ameweka bayana sababu ya kuvaa vazi analosema ni kama mtindo wa nguo anazopenda kuvaa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Nandy aliyevalia vazi hilo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari leo kuhusu tamasha lake la Nandy Festival litakalofanyika Mwanza kesho, alikuwa amevaa ushungi mweusi na vazi la suti nyekundu aina ya Kaunda.

Baada ya kuulizwa kuhusu uvaaji wa vazi hilo ikiwa ni mara yake ya kwanza akiwa katika muonekano huo, amesema anavutiwa sana na uvaaji huo wa Rais Samia, kiasi cha yeye kuamua kuiga akisema ni vazi zuri kwa wanawake.

“Rais amevaa vazi hilo la kipekee ambalo ni zuri na wanawake kwa sasa wanavaa, nikaona na mimi niwakilishe. Nitaenda kwenye tamasha la Nandy kisamia, huu ni mwanzo tu mtaona nikivaa zaidi ya hapa ”amesema Nandy

Related Articles

Back to top button