Mastaa

Ben Affleck aweka wazi sababu ya kuachana na Jennifer Lopez

NEW YORK: TALAKA ya waigizaji Ben Affleck na Jennifer Lopez ilitawala vichwa vya habari kote ulimwenguni kwa miezi kadhaa mwaka jana.

Mastaa hao wawili wa Hollywood waliachana miaka miwili tu baada ya kufunga pingu za maisha, na tangu wakati huo, wamekuwa na sintofahamu kuhusu kutengana kwao. Lakini katika mahojiano mapya na GQ, Ben Affleck amefunguka kuhusu kuachana kwao.

Akizungumzia sababu za ndoa yake kuvunjika, muigizaji na muongozaji wa sinema Ben Affleck amesemaa, hataki ulimwengu ufikirie kuwa anamfikiria vibaya Jennifer kwa sababu tu hawako pamoja tena.

“Sina chochote ila heshima. Nadhani kuna tabia ya kuangalia talaka na kutaka kutambua sababu kuu au kitu. Lakini kusema ukweli, kama nilivyosema, ukweli ni wa kunukuu zaidi kuliko pengine watu wangeamini au ungependeza,” ameongeza.

Ben Affleck amesema hakuna kitu kilichosababisha waachane kama wengi wanavyodhani bali ni namna ya maisha yao waliyokuwa wakiishi huku kila mmoja akijaribu kumuelewa mwenzake.

Ben Affleck na Jennifer Lopez walichumbiana mwanzoni mwa miaka ya 2000 na kuachana kwa talaka mnamo Agosti 2024.

Related Articles

Back to top button