Ligi Kuu

Diarra kukiwasha dhidi ya Mbeya City

DAR ES SALAAM: KIPA namba moja wa Yanga, Djigui Diarra atarajiwa kuonekana tena uwanjani baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungimiwa michezo mitatu.

Nyota huyo huenda akarejea uwanjani katika mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Alhamis kwenye Uwanja wa KMC.

Diarra alitumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu ambayo ni dhidi ya Tanzania Prisons, Pamba Jiji na TMA.

Wakati Diarra akirejea, Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga Ally Kamwe, amesema mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City unahitaji nguvu ya mashabiki kwa wingi Uwanjani ili kulipiza kisasi.

Kamwe amekumbushia namna Mbeya City ilivyowabana mbavu katika mchezo wa mzunguko wa kwanza kwa kutoka sare akisema ili kubakiza pointi tatu nyumbani kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake.

Mchezo huo unatarajia kuchezwa kwenye Uwanja wa KMC Dar es Salaam Alhamis ya April 15, mwaka huu.

“Kipaumbele chetu tumeelekeza mchezo ujao dhidi ya Mbeya City, tunakumbuka walivyotubana mbavyu katika mchezo wa kwanza. Sasa ili kushinda mchezo huu tunahitaji mashabiki kujitokeza kwa wingi kuunga mkono,”amesema.

Kamwe amesema ni muhimu kwa mashabiki kuwa sehemu ya kikosi hicho kwa kutoa hamasa kubwa, akisisitiza kuwa benchi la ufundi tayari limekamilisha maandalizi ya wachezaji, hivyo jukumu lililobaki ni kwa mashabiki kwenda kuisapoti timu ili kupata matokeo mazuri.
Aidha, amebainisha kuwa Yanga SC inakuja kwenye mchezo huo ikiwa na morali kubwa baada ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho, hali inayoongeza hamasa zaidi kwa wachezaji na mashabiki kuelekea mchezo huo muhimu.
Mwisho

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button