Ligi Kuu

Lyanga: Tunahitaji ushindi kujiweka nafasi nzuri

SINGIDA: MSHAMBULIAJI wa Singida Black Stars, Ayoub Lyanga, amesema kikosi chao kimejiandaa vizuri kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons, huku akisisitiza kuwa wachezaji wote wana morali kubwa ya kuhakikisha wanapata ushindi.

Lyanga amesema wanafahamu ugumu wa mchezo huo kutokana na Tanzania Prisons kupambana kuboresha nafasi yao kwenye msimamo wa ligi, lakini Singida Black Stars pia ina malengo makubwa ya kumaliza msimu katika nafasi nzuri na kufuzu mashindano ya CAF.

“Kwa upande wa wachezaji, tumejiandaa vizuri na morali ni kubwa kuelekea mchezo wa kesho. Tunajua mchezo utakuwa mgumu kwa sababu Tanzania Prisons wanahitaji pointi, lakini nasi tunahitaji ushindi kwa sababu tuko nyumbani na tunapigania malengo makubwa.”

Mshambuliaji huyo amesema anajisikia vizuri kwa sasa na yuko tayari kuendelea kuipambania timu yake kila anapopewa nafasi ya kucheza.

“Ninajisikia vizuri na niko tayari kuisaidia timu. Kila mmoja wetu amejipanga kuhakikisha tunafikia malengo ambayo klabu imejiwekea msimu huu.”amesema.

Aidha, amewashukuru mashabiki wa Singida Black Stars kwa sapoti wanayoendelea kuipa timu na kuahidi kuwa wachezaji watajituma kwa nguvu zote kuhakikisha wanapata matokeo mazuri mbele yao.

Related Articles

Back to top button