Tetesi

Nketiah kuondoka Arsenal

TETESI za mpira wa miguu zinasema mshambuliaji wa England, Eddie Nketiah, 24, anaweza kuondoka Arsenal majira yajayo ya kiangazi kufuatia nia kumsajili toka Crystal Palace, Brentford na Wolves. (Football Insider)

Manchester United ipo tayari kuimarisha nia kumsajili beki mbrazil wa Juventus, Gleison Bremer, 27, ambaye ana kipengele cha kuachiwa cha pauni mil 43 katika mkataba wake. (Mirror)

Huenda Aston Villa ikalazimika kumuuza kiungo mwingereza Jacob Ramsey, 22, kusaidia kuepuka kuvunja kanuni za faida na uendelevu za Ligi Kuu England. (Football Insider)

Beki wa kulia wa Monaco Vanderson anatarajiwa kupokea ofa kadhaa majira yajayo ya kiangazi huku Barcelona, Real Madrid na Manchester United zikionesha nia kupata saini yake mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Fichajes – Spain)

Chelsea imeonesha nia kumsajili fowadi wa Barcelona Ferran Torres, ambaye anatarajiwa kupatikana kwa bei sahihi. (Fichajes – Spain)

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button