Tetesi

Al Ittihad kumsajili Salah kwa Bil 647/-

TETESI za usajili zinasema klabu ya Al Ittihad ya Saudi Arabia iko tayari kuvunja rekodi ya dunia ya uhamisho kwa dau la pauni 216 sawa na shilingi bilioni 647.3 kumnunua mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah mara tu dirisha la usajili la Januari, 2024 litakapofunguliwa.(Fichajes)

Mshambuliajii wa Napoli, Victor Osimhen anatarajiwa kuwekewa dau la pauni milioni 173 kutoka timu nyingine ya Saudi Arabia, Al Hilal. Chelsea na Real Madrid zote zina nia kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria.(Gazzetta dello Sport)

Liverpool inaangalia uwezekano wa kumsajili winga wa Borussia Dortmund, Donyell Malen, ambaye klabu hiyo ya Ujerumani inamthaminisha kuwa pauni milioni 52.(BILD)

Chelsea inajiandaa kupokea ofa kutoka klabu mbalimbali kwa ajili ya kumsajili beki wa kushoto Marc Cucurella, Januari 2024. Real Madrid ipo tayari kufikia dili hilo kwa mkopo. (ESPN)

Related Articles

Back to top button