Ligi Kuu

Vita ya Simba, Yanga asiingilie mtu!

DAR ES SALAAM: WAKATI tofauti ya alama moja mbele ya Mpinzani wao Simba, klabu ya Yanga sasa wanachokifanya ni kushinda idadi kubwa ya mabao katika kila mechi.

Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 6-1dhidi ya Ken Gold katika mchezo wa leo uliochezwa uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge.

Mshambuliaji wa Yanga, Prince Dube amefunga bao la kwanza na tano dakika ya 2 na 46, Clement Mzize amepata bao la pili na nne dakika ya 6 ya 42 pasi kutoka kwa Stephen Aziz Ki.

Kiungo Mshambuliaji Pacome Zouzoua amepata bao la 3 dakika ya 39 pasi kutoka kwa Dube, Duke Abuya ameipatia bao la sita dakika ya 85 akiunganisha pasi ya Kennedy Musonda.

Bao la Kwanza la Kengold limefungwa na Selemani Rashid dakika ya 86 baada ya kupiga shuti kutoa kati ya uwanja na kipa wa Yanga,  Djigui Diarra kumsinda mpira na kuingia nyavuni.

Related Articles

Back to top button