Arteta awaweka Chelsea kwenye mbio za ubingwa

LONDON: Bosi wa Arsenal Mikel Arteta amewatabiria makubwa wapinzani wake wa jiji moja Chelsea kwa kusema kuwa the blues watakuwa miongo mwa timu zinazowania ubingwa msimu huu.
Arteta ambaye atakutana na Chelsea katika mchezo wa ligi kuu ya England Jumapili amesema staili ya uchezaji ya Chelsea ni ya kutia matumaini na watu wasiwabeze na kuwaondoa kwenye wawania taji la ligi hiyo msimu huu.
“Tangu nilivyowaona kwenye pre season na ninavyojua utendaji kazi wa Enzo (Maresca) na aina ya wachezaji waliopo kikosini ni washindani wazuri wa ubingwa wa ligi tangu mwanzo”
“Wana vitu vingi kikosini najua mara tu watakapotulia na kupata ule muunganiko wao, nguvu na consistency nadhani wanaweza kushindana na timu yangu” amesema Arteta
Chelsea na Arsenal watakiwasha mapema Jumapili hii katika dimba la Emirates jijini London saa 10:30 saa za Afrika Mashariki wakiwa na kumbukumbu ya sare ya bao 1-1 katika dimba la Stamford Bridge.
Chelsea hawajaifunga Arsenal katika michezo mitano iliyopita, wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kipigo cha mabao 5-0 Aprili mwaka jana. Wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa nyuma ya Arsenal walio nafasi ya pili kwenye msimamo kwa pointi sita.