Arsenal kusaka ‘straika’ Januari hii

LONDON:MENEJA wa Arsenal Mikel Arteta amesema kikosi chake kitaingia sokoni Januari hii kusaka mshambuliaji baada ya Mbrazili Gabriel Jesus na winga Bukayo Saka kupata majeraha hivi karibuni.
Kwa mara nyingine tena Arsenal walishinda 2-1 kwenye mchezo wa dabi dhidi ya Tottenham Hotspur hapo jana, licha ya kuonekana wazi kikosi hicho kinahitaji mshambuliaji asilia. Alipoulizwa baada ya mchezo iwapo atalimulika eneo hilo, Arteta alijibu
“Kwakweli ndio, kwa sababu tumepoteza wachezaji wawili muhimu sana Bukayo ambaye hatakuwepo kwa miezi mitatu halafu Gabby (Gabriel Jesus) tutamkosa kwa muda mrefu sana. Hivyo ndio tutajaribu, tunatafuta tuone tutakachopata”
Arsenal wamefufua tena matumaini ya kurejea kwenye mbio za ubingwa wa Ligi kuu ya England baada ya ushindi wa huo wa jana na wachambuzi nchini England wanaamini iwapo Arsenal watasajili mshambuliaji asili.