Mastaa

Arnold Schwarzenegger bega kwa bega na Kamala Harris

WASHINGTON: LICHA ya wasanii kadhaa kukataa kuingia katika siasa kwa madai ya kutotaka kuwatenga mashabiki wao, muigizaji na gavana wa zamani wa California, Arnold Schwarzenegger ametangaza kuwa upande wa Makamu wa Rais na mgombea wa Chama cha Democratic, Kamala Harris huku akidai kuwa ndiye anatakiwa kuwa rais wa Marekani kwa sababu anajitolea mno kwa nchi.

“Siku zote nitakuwa Mmarekani kabla ya kuwa Republican,” Schwarzenegger aliandika katika mtandao wake wa kijamii. “Ndio maana, wiki hii, ninampigia kampeni na nitampigia kura Kamala Harris na Tim Walz.”

Schwarzenegger, ambaye alitawala California kutoka 2003 hadi 2011, amekuwa akikosoa sera za Donald Trump kwa muda mrefu.

Katika taarifa yake, Schwarzenegger pia alikosoa kukataa kwa rais wa zamani wa Marekani Trump kupinga matokeo ya uchaguzi wa 2020, akisema ” Marekani haipo hivyo, Marekani anayeshindwa anakubali na anampisha mwezake kwa amani.”

“Kwa mtu kama mimi ambaye anazungumza na watu kote ulimwenguni na bado anaita Marekani kuwa pipa la takataka huyo sio mzalendo. Inanikera,” Schwarzenegger alisema.

Katika nafasi ya pili ya urais wa Trump, amesema: “Atagawanya, atatukana, atapata njia mpya za kuwa Mmarekani zaidi ya vile alivyokuwa tayari, na sisi, watu, hatutapata chochote isipokuwa hasira zaidi juu yake hivyo hafai.

“Hiyo ni sababu tosha kwangu kushiriki kura yangu na ninyi nyote. Nataka kusonga mbele kama nchi, kura yangu ni kwa Kamala Harris na Tim Walz” aliongeza.

Related Articles

Back to top button