Ariana Grande kuachia albamu mpya mwezi huu

NEW YORK: MWANAMUZIKI na muigizaji mwenye umri wa miaka 31 Ariana Grande baada ya kufanya vizuri katika filamu ya ‘Wicked’ sasa ametanga kurudi upya katika muziki wake kwa kutoa albamu ndani ya mwezi huu.
Katika tangazo lake kupitia ukurasa wake wa Instagram wiki hii, ametangazaujio wa ‘Eternal Sunshine Deluxe: Brighter Days Ahead’ akimaanisha ataachia wimbo mpya na albamu Machi 28 ikiwa na nyimbo sita mpya.
Akizungumza kwenye podikasti ya ‘Las Culturistas’, amesema: “Iko moyoni mwangu.
“Nitasema jambo la kutisha sana litawatisha mashabiki wangu na kila mtu, lakini ninawapenda, na watashughulikia, na tutakuwa hapa milele.
“Siku zote nitafanya muziki, nitapanda jukwaani, nitafanya vitu vya pop, naahidi.
“Lakini sifikirii kuifanya kwa kiwango ambacho nimekuwa nikifanya kwa miaka 10 iliyopita ndipo ninapoona miaka 10 ijayo.”
Ariana hajatoa wimbo tangu tafrija yake ya ‘Sweetener’, licha ya kuachia ‘Thank U, Next’ (2019) na ‘Positions’ (2020) wakati alipofanya ziara yake ya mwisho.
Rekodi katika lebo inayosimamia kazi zake ilijibu kupitia mtandao wa X zamani Twitter kwamba: “Hakuna mipango ya ziara kwa mwaka ujao, lakini Ariana amewashukuru sana mashabiki wake kwa upendo unaoendelea kwake.”