FM Academia,Bella, Twanga Peteta kukiwasha
Msimu wa tatu wa Grand Gala Dance unatarajiwa kufanyika Agosti 30, 2024 katika ukumbi wa The Super Dome Masaki uliopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo muandaaji wa tukio hilo, Mboni Masimba amesema kuwa Grand Gala Dance itapambwa na burudani kutoka kwa bendi nne ikiwemo FM Academia.
“Usiku wa Grand Gala Dance umeanzishwa mahususi kwa ajili ya kumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na utakuwa na burudani kutoka kwa Bendi ya FM Academia, Christian Bella, Twanga Peteta na Tukuyu Sound,”amesema.
Naye Pancho Mwamba amesema kuwa wananchi watarajie muziki mzuri kutoka kwa Bendi ya FM Academia huku akisisitiza kuwa sio mashindano bali ni muziki mzuri kutoka kwao kauli iliyoungwa mkono na msanii Christian Bella ambaye amesema anajipanga kutoa burudani ya aina yake.