Aprili katili kwa Liverpool

Mwezi Aprili utakaoanza saa chache zijazo utakuwa wa kikatili kwa Liverpool kutokana na kukabibiliwa na michezo migumu ya Premier League katika siku tisa za mwanzo za mwezi.
Liverpool iliyopo nafasi ya 6 katika msimamo wa EPL ikiwa na pointi 42 ipo katika wakati mgumu kupigania kufuzu nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Michezo saba itakayocheza Liverpool katika siku 30 zijazo ni pamoja na mechi dhidi ya Manchester City, Chelsea, Arsenal na Tottenham HotSpur.
Mechi za Liverpool kwa mwezi Aprili ni kama ifuatavyo:
Liverpool vs Manchester City-Aprili 1
Chelsea vs Liverpool– Aprili 4
Liverpool vs Arsenal- Aprili 9
Leeds United vs Liverpool – Aprili 17
Liverpool vs Nottigham Forest–Aprili 22
West Ham United vs Liverpool –Aprili 26
Liverpool vs Tottenham HotSpur–Aprili 30