Filamu

Angelina Jolie, Brad Pitt waafikiana kuhusu talaka 

NEW YORK: WAIGIZAJI nyota wa Hollywood, Angelina Jolie na Brad Pitt wamefikia makubaliano ya talaka kufuatia vita vya kisheria vya miaka minane, kulingana na wakili wake.

Wawili hao waliofunga ndoa mwaka 2014 na kupata watoto sita, walikuwa miongoni mwa wapenzi wenye hadhi ya juu katika tasnia ya burudani kiasi kwamba walipewa jina la utani la ‘Brangelina’ kutokana na mapenzi yao.

Jolie aliwasilisha kesi ya talaka mnamo 2016, akitaja “tofauti zisizoweza kusuluhishwa.” Baadaye iliibuka wakati wa taratibu tofauti za mahakama kwamba alimshtaki Pitt kwa kumdhulumu yeye na watoto wao wawili kwenye ndege ya kibinafsi mwaka huo wa 2016.

Pitt hakufunguliwa mashtaka kufuatia uchunguzi wa polisi kuhusu tukio hilo na amekanusha madai hayo.

Hata hivyo licha ya kufikia makubaliano hayo mawakili wake hawajatoa maoni yao hadharani kuhusu suluhu ya talaka hiyo.

Wanandoa hao walikuwa wamejiingiza katika vita vya kulea mtoto katika miezi iliyofuata tangazo lao la talaka. Walikubaliana na mpango wa pamoja mnamo 2021.

Wakati mawakili wa Jolie wakisema suluhu ya talaka imefikiwa, haijabainika iwapo itamaliza vita vingine vya kisheria kati ya wawili hao kuhusu shamba la mizabibu la Ufaransa na madai mengine ya unyanyasaji.

Angelian na Brad Pitt wamehusika katika mzozo unaoendelea kuhusu Chateau Miraval, ambayo walinunua pamoja mnamo 2008 ambapo harusi yao ingefanyika.

Mnamo 2022, Pitt alimshutumu Jolie kwa kuuza hisa yake katika mali hiyo kwa oligarch wa Urusi, Yuri Shefler bila yeye kujua. Jolie hakutoa maoni yake hadharani kuhusu kesi hiyo wakati huo.

Wanandoa hao waliingia katika mahusiano ya ndoa baada ya kufanya filamu ya pamoja mwaka 2005 ya ‘Mr and Mrs Smith’ na uhusiano wao ukavutia vyombo vya habari vya kimataifa.

Ndoa hiyo ilikuwa ya pili kwa Pitt baada ya uhusiano na nyota wa Friends, Jennifer Aniston. Ilikuwa ya tatu kwa Jolie, baada ya waigizaji Billy Bob Thornton na Jonny Lee Miller.

Jolie aliigiza katika filamu ya ‘Lara Croft: Tomb Raider’, ‘Changeling na Girl’, ‘Interrupted’ na filamu yake ya mwaka huu ni ‘Maria’ inayohusu mwimbaji wa opera Maria Callas.

Pitt naye hakuwa nyuma kwa mwaka huu amecheza filamu ya ‘Once Upon a Time in Hollywood’ na ‘Monkeys 12’ na pia ameonekana huko Silverstone mwaka huu akirekodi filamu yake ya ‘Formula One’ inayoitwa ‘F1’, ambayo atacheza na mkongwe Sonny Hayes.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button