Habari Mpya
Kisa busu, Rubiales atozwa milioni 27

MADRID: Mahakamani nchini Hispania leo Feb 20 imemkuta na hatia ya kupiga busu bila ridhaa rais wa zamani wa shirikisho la soka nchini humo(RFEF) Luis Rubiales
Rubiales alifunguliwa mashtaka mahakamani hapo baada ya kumbusu mchezaji wa timu ya taifa ya Wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa kombe la dunia la Wanawake la Agosti mwaka 2023 nchini Australia.
Mahakama imemuamuru Rubiales kulipa faini ya zaidi ya Euro elfu 10 ambazo ni sawa na milioni 27 za Kitanzania, huku ikielezwa waendesha mashtaka walitaka afungwe jela. Awali rais huyo wa zamani wa shirikisho la soka nchini Spain alikana kulazimisha busu hilo akisema kuwa Hermoso aliruhusu.