Tetesi

Man U wamganda De Ligt

MANCHESTER: Miamba ya jiji la Manchester, Wekundu wa Old Trafford Manchester United bado wana mpango wa kunasa saini ya beki wa kimataifa wa Nederlands na Bayern Munich Matthijs de Ligt licha ya kumtaka Branthwaite kama mbadala.

De Ligt anasalia kuwa kipaumbele cha mashetani Wekundu, huku makubaliano yakikaribia kufikiwa na taarifa zikieleza kuwa masharti ya binafsi ya mchezaji huyo na wakala wake Pimenta anayeshughulikia mpango huo yanajadiliwa.

Inaelezwa kuwa mazungumzo hayo yanaendelea vizuri kwa sababu De Ligt anaonesha nia ya dhati ya kuhama na Bayern na kujiunga na Manchester united iliyomaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa EPL msimu uliopita na tayari pande hizo mbilj zinajadili muundo na ada ya uhamisho wa beki huyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button