Ligi KuuNyumbani

Azam Fc yashusha mwingine

AZAM FC  imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao baada ya leo Julai 5, 2023 kumtambulisha kocha msaidizi kikosini hapo.

Miamba hiyo ya kusini mwa Dar es Salaam imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitatu na kocha Mfaransa Bruno Ferry.

Kwenye taarifa iliyotolewa na Azam Fc kupitia kurasa zake za mitandao imesema

“Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka mitatu na Bruno Ferry atakayekuwa kocha msaidizi”

Kocha huyo mwenye miaka 56, atasaidiana  na kocha mkuu wa timu hiyo youssouph Dabo kukisuka kikosi hicho msimu ujao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button