Lulu Diva na D voice wasambaza video za harusi yao

DAR ES SALAAM: WASANII wa muziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva na Dvoice, wamefunga ndoa baada ya kudumu katika mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi cha miaka miwili.
Ndoa hiyo imefungwa katika hafla ya faragha iliyohudhuriwa na ndugu na jamaa wa karibu kutoka katika familia zote mbili, huku wawili hao wakichukua hatua mpya katika maisha yao ya pamoja.
Lulu Diva na Dvoice wamekuwa miongoni mwa wapenzi waliozungumziwa katika tasnia ya burudani, hasa kutokana na tofauti ya umri kati yao.
Dvoice ana umri wa miaka 24, huku Lulu Diva akiwa na miaka 34, hali inayowafanya kutofautiana kwa miaka 10.
lHatua hiyo imefungua ukurasa mpya katika maisha yao, huku wakipokea pongezi kutoka kwa mashabiki na wadau wa burudani.
Hongera Lulu Diva na Dvoice kwa kufunga ndoa na kuanza safari mpya ya maisha ya pamoja!




