Nyumbani

Simba kucheza mechi zote Uhuru

DAR ES SALAAM: SIMBA imetangaza rasmi ratiba ya michezo yake miwili dhidi ya FC 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta katika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), huku mechi zote zikitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ratiba hiyo imetangazwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, leo ikieleza kuwa mchezo wa kwanza utachezwa Oktoba 20, 2026, huku wa marudiano ukipangwa Oktoba 25, mwaka huu.

Awali, mchezo wa kwanza ulipangwa kuchezwa nje ya Tanzania, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo), kabla ya ratiba kubadilika na michezo yote miwili kuhamishiwa Uwanja wa Uhuru.

Kwa Simba, michezo hiyo ni muhimu katika harakati za kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo ushindi wa jumla dhidi ya FC 15 de Agosto utaiwezesha kusonga mbele katika mashindano hayo.

Simba italazimika kutumia vizuri nafasi ya kucheza nyumbani katika michezo yote miwili ili kutimiza lengo hilo, huku ikihitaji kupata matokeo mazuri katika mikondo yote miwili ya pambano hilo.

Related Articles

Back to top button