Nyumbani

Msigwa amshukuru Samia kuelekea AFCON 2027

Maandalizi ya Afcon 2027 yamefikia pazuri

DAR ES SALAAM: KATIBU Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kupata fedha za kutosha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya michezo.

Amesema tayari uwanja wa Arusha utakaoingiza mashabiki 30,000 ujenzi wake unaendelea lakini kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kujenga viwanja vya mazoezi Zanzibar, Dar es Salaam na Arusha kwa ajili ya AFCON 2027.

Ameongea hayo akiwa Mgeni rasmi katika usiku wa tuzo za wanamichezo bora wa msimu wa 2023/24 zilizoandaliwa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, zilizofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki.

“Ukiwa na miundombinu mibovu huwezi kujinasibu tumepiga hatua katika michezo, kufanya vizuri katika michezo ni kuwepo kwa miundombinu bora.

Taasisi binafsi zinatakiwa kuwekeza katika miundo mbinu katika michezo mbalimbali na isiwe soka pekee, ukizingatia katika kuogelea Collins Saliboko amefanya vizuri kwenye Olimpiki lakini hakuna bwawa lenye mita 50 hapa nchini lakini ameweza kuweka rekodi nzuri.,” amesema Msigwa.

Amewaomba  wawekezaji kuwekeza katika vituo vya akademia kwa sababu kipaji ni sawa, lakini zama zake zinakufa kwani dunia ya sasa kipaji kinaenda sambamba na  taaluma pamoja na nidhamu.

“Wadau naombeni kudhamini michezo , tukifanya hivyo tutawezesha maeneo yote ya nchi yetu. Kuna vijana katika  maeneo mengine hawapati fursa hiyo wafikiwe na kuweza kupata wachezaji wazuri. Tusiache majukumu ya kulea wanamichezo, utakuta mwaka huu wamefanya vizuri,  mwakani wanapotea,” amesema Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Msigwa.

 

 

Related Articles

Back to top button