Nyumbani

Simba yasubiri uamuzi wa CAF kuhusu De Agosto

DAR ES SALAAM: SIMBA SC imesema inasubiri uamuzi wa mwisho wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuhusu mahali pa kuchezwa kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya De Agosto, baada ya wapinzani hao kuomba mechi hiyo ichezwe nchini DR Congo badala ya Dar es Salaam.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema awali klabu hiyo ilifanya mawasiliano na De Agosto ili kufahamu mahali ambapo mchezo wa kwanza ungechezwa kutokana na changamoto za viwanja zinazowakabili wapinzani hao.

Amesema kutokana na kutopata majibu kwa wakati, Simba iliamua kuwasiliana na CAF ili kupata ufafanuzi kuhusu mahali pa kuchezwa kwa mchezo huo.

Ahmed amesema CAF nayo iliwasiliana na De Agosto kabla ya kutoa maelekezo kwamba mechi zote mbili, ya kwanza na ya marudiano, zichezwe jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa maelekezo hayo, De Agosto wangetumia Dar es Salaam kama uwanja wao wa nyumbani katika mchezo wa kwanza, huku Simba ikiwa mwenyeji wa mchezo wa marudiano katika jiji hilo hilo.

Hata hivyo, Ahmed amesema baada ya maelekezo hayo kutolewa, wapinzani wao wameanza tena kufanya mawasiliano na CAF wakitaka mchezo wao wa kwanza uhamishiwe nchini DR Congo.

Amesema Simba inasubiri maamuzi ya mwisho kutoka CAF kabla ya kutoa taarifa rasmi kwa mashabiki wake kuhusu mahali ambapo mchezo huo utachezwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button