Nyumbani

‘Faili’ la Simba, Yanga, Azam latua kwa Profesa Janabi

DAR ES SALAAM: MKURUGEZI Mtendaji wa Hospita ya Taifa ya Muhimbili, Profesa, Mohamed Janabi amezigeukia Yanga, Simba, Azam FC na Coastal Union, kuzingatia zaidi vipimo makini kwa wachezaji wapya watakawasajili kwa msimu wa 2023\24.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwezo wa hospital ya Muhimbili kampasi ya Mloganzila, katika zoezi la kumuaga mchezaji wa zamani wa Yanga, Sunday Manara ambaye ameruhusiwa kutoka Hospitali baada ya matibabu katika hospitali hiyo ambakoi amefanyiwa upasuaji wa goti.

Profesa Janabi amezitaka klabu hizo ambazo zinaenda kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimatifa, Yanga na Azam FC wakicheza Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba na Coastal Union wakicheza Kombe la Shirikisho.

Amesema klabu hizo zinatakiwa kuwekeza zaidi katika suala la kupima afya za wachezaji wanaowasajili kwa kuangalia maeneo makuu mawili ambayo ni utimamu wa afya ya magoti na moyo.

“Hizi klabu zinatumia fedha nyingi sana kusajili wachezaji hao wa kigeni, kabla ya kuwapa mkataba wanalazimika kuwapima afya zao, Mlonganzila tupo tayari kuangalia afya za wachezaji hao wanaowasajili”.

“Mfano ni hivi karibuni tumeona moja ya klabu hizi haikuweza kumtumia mchezaji wake aliyesajiliwa kwa gharama kubwa na kucheza mechi moja au mbili na kukosa msimu mzima,” amesema Profesa Janabi.

Amesema viongozi wa klabu hizo wasidanganyike na ‘Clip’ za YouTube wanazotumiwa kuangalia wachezaji wao kwa ajili ya kuwasajili na kutakiwa zaidi kuwapima afya ikiwemo magoti na vipimo vya moyo.

Related Articles

Back to top button