Kwingineko

Suzuki aazimia kufuta kumbukumbu mbaya za Asian Cup

TOKYO: Kipa wa Aston Villa na timu ya taifa ya Japan, Zion Suzuki, amesema yuko tayari kutumia uzoefu alioupata katika miaka ya hivi karibuni kuisaidia Japan kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Asia (Asian Cup) yatakalofanyika Saudi Arabia mwakani.

Suzuki, mwenye miaka 24, bado anakumbuka makosa aliyofanya katika michuano ya Asian Cup mwaka 2024 nchini Qatar, ambapo Japan ilitolewa katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Iran.

Kipa huyo amesema wakati huo hakuwa katika kiwango kizuri na anajilaumu mno kwa kipindi kile.

 

“Wakati ule nilikuwa nacheza kwa mara ya kwanza na nilicheza vibaya sana. Nilihisi kwamba nilichangia timu kushindwa,” alisema Suzuki baada ya Japan kuifunga New Zealand mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika jiji la Tokyo.

Lakini safari hii anaingia kwenye michuano akiwa na uzoefu mkubwa zaidi. Suzuki amecheza Kombe la Dunia na sasa anashiriki Ligi Kuu ya England akiwa na Aston Villa, jambo analosema limemjengea kujiamini.

“Safari hii nimepitia mambo mengi. Nimecheza Kombe la Dunia na sasa nacheza Premier League, hivyo ninajiamini zaidi,” alisema.

Suzuki pia amesema anaamini Japan inaweza kushinda Asian Cup baada ya kusubiri kwa miaka 16 bila kutwaa taji hilo.

“Nataka kuisaidia timu na tunaamini tunaweza kushinda Asian Cup,” alisema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button