Muziki

Taylor Swift, Beyonce wamuaga mkongwe Dolly Parton

LOS ANGELES: MASTAA wakubwa wa muziki duniani, Taylor Swift na Beyoncé, wameungana na wasanii wengine kutoa salamu za heshima kwa gwiji wa muziki wa country, Dolly Parton, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Parton, ambaye alikuwa mmoja wa wasanii mashuhuri zaidi katika historia ya muziki wa Marekani, kiasi kwamba rais wan chi hiyo aliamuru maombolezo kwa nchi nzima kutokana na kifo cha mkongwe huyo aliyefariki Agosti 25, 2026 baada ya kukabiliwa na maradhi ya saratani. Kifo chake kimezua maombolezo makubwa katika tasnia ya burudani duniani.

Taylor Swift katika ujumbe wake wa maombolezo alieleza kuwa dunia bila Dolly Parton inaonekana kuwa kitu kisichowezekana, huku akimsifu kwa kuwa mtu mwenye neema, ujasiri na moyo wa kuwasaidia wengine.

Swift pia alieleza namna Parton alivyowatia moyo wasichana wengi kufuata ndoto zao na kuwa wao wenyewe, akisisitiza kuwa urithi wake utaendelea kuishi kupitia muziki na kazi zake za kusaidia jamii.

Kwa upande wake, Beyoncé, ambaye aliwahi kushirikiana na Parton kwenye wimbo “Jolene” kupitia albamu yake Cowboy Carter, alimtaja Parton kama mtu aliyekuwa nyota ya kuwaongoza wengine, akimsifu kwa ubunifu, ujasiri na uwezo wake wa kuwa tofauti.

Mbali na Swift na Beyoncé, mastaa wengine waliotoa heshima zao ni pamoja na Miley Cyrus, Paul McCartney, Celine Dion, Jane Fonda, Reba McEntire na wengine wengi.

Dolly Parton anakumbukwa kwa nyimbo maarufu kama “Jolene” na “I Will Always Love You”, pamoja na mchango wake mkubwa katika muziki, filamu na shughuli za kijamii.

Related Articles

Back to top button