Muziki

Mbosso kuzindua EP mpya ‘room number 3’ kesho

MSANII maarufu wa Bongo Fleva, Mbosso Khan, anatarajiwa kuachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Room Number 3 kesho, chini ya lebo yake mpya, Khan Music.

Kwa siku kadhaa sasa, Mbosso amekuwa akiwapa mashabiki wake dokezo kupitia picha na video zenye mandhari ya kijani kibichi, alama ya RN3, pamoja na sauti za watoto wake wakimtambulisha kwa upendo kama “Baba Yetu”.

Katika kuendeleza kampeni hiyo, leo jioni kuanzia saa 12, Mbosso atafanya Exclusive Listening Party ya EP hiyo ndani ya Century Cinemax, Mlimani City. Ni hafla maalum kwa watu wachache waliopata nafasi ya kipekee kusikiliza nyimbo hizo kabla hazijaachiwa rasmi kwa umma.

Room Number 3 inatajwa kuwa ni ishara ya mwanzo mpya kwa Mbosso katika safari yake ya muziki — akiwa na uhuru wa kisanii, uelekeo mpya binafsi, na dhamira ya kuandika sura mpya kupitia kazi zake.

Mashabiki wa Mbosso wameshaanza kuonesha hamasa kubwa, wakisubiri kusikia sauti mpya ya msanii huyo ambaye amedumu kwa muda mrefu chini ya lebo ya WCB Wasafi kabla ya kuanzisha Khan Music.

 

Related Articles

Back to top button