Kwingineko

Bandari FC yajigamba kubeba Kombe la Kenya, Kocha atoa neno

MOMBASA, KENYA : KOCHA mkuu wa Bandari FC, Charles Okere, amesema kikosi chake kiko tayari kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL), huku akilenga kuiongoza timu hiyo kuvunja ukame wa mataji.

Bandari FC inatarajiwa kuanza kampeni yake ya msimu mpya mwishoni mwa wiki dhidi ya AFC Leopards, baada ya kukamilisha maandalizi yake ya msimu kwa ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Dola Select katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana Agosti 25, 2026 kwenye Uwanja wa Mbaraki.

Okere amesema maandalizi ya timu yamekwenda vizuri, huku wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri kiafya bila kupata majeraha makubwa.

“Wachezaji wote wako fiti na jambo muhimu ni kwamba tuko tayari kwa mchezo dhidi ya AFC mwishoni mwa wiki. Nimefurahishwa na uongozi wa timu kwa kutupa muda wa kutosha wa maandalizi na ninaamini tutakuwa na msimu mzuri,” alisema Okere.

Hata hivyo, kocha huyo ameelezea wasiwasi wake kuhusu sintofahamu inayozunguka kuanza kwa msimu mpya, akisema mzozo wa kisheria unaoendelea umeathiri maandalizi ya timu mbalimbali.

“Tunajua tuna mchezo wa kwanza wa msimu mpya mwishoni mwa wiki. Tunachosubiri ni uamuzi wa mahakama, lakini hali hii ya kusubiri na kutokuwa na uhakika si nzuri kwa soka letu.

Related Articles

Back to top button