Ligi Kuu

Moallin: Changamoto zimetumarisha

DAR ES SALAAM: Kocha wa Yanga, Abdi Hamid Moallin, amesema msimu wa 2025/26 ulikuwa mrefu na wenye changamoto nyingi, lakini changamoto hizo zimeifanya timu kuwa imara zaidi na hatimaye kufanikiwa kutwaa ubingwa wa tano mfululizo.

Akizungumza Dar es Salaam Moallin amesmea kwa sasa anaelekea mapumzikoni baada ya msimu kumalizika, huku uongozi wa klabu ukiendelea na maandalizi ya msimu ujao.

“Ulikuwa msimu mrefu na wenye changamoto nyingi. Lakini kupitia changamoto unakua na kuwa imara zaidi. Mwishowe tulifanikiwa kutwaa ubingwa wetu wa tano mfululizo, jambo ambalo linatupa furaha kubwa.” Amesema.

Akizungumzia msimu ujao, Moallin amesema Yanga italazimika kujiandaa vizuri kutokana na majukumu ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kila timu hutumia kipindi hiki kujiimarisha. Sisi pia tutafanya hivyo ili kuwa na kikosi bora kitakachoweza kukabiliana na majukumu yote ya msimu ujao.”ameongeza.

Kuhusu hali ya kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua, kocha huyo amesema mchezaji huyo alifanyiwa upasuaji kwa mafanikio usiku uleule aliopata majeraha na anaendelea vizuri na matibabu.

Moallin alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kumtembelea Pacome hospitalini, akisema hatua hiyo inaonesha jinsi anavyojali maendeleo ya michezo na ustawi wa wachezaji.

Related Articles

Back to top button