Hersi, Arafat wapeta mchujo Yanga

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga imetangaza orodha ya wagombea waliopita katika mchujo wa awali wa uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo, huku Rais wa sasa, Hersi Said, akipitishwa kuwania tena nafasi ya urais.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Malangwe Mchungahela, mgombea Arafat Haji naye amepitishwa kuwania nafasi ya Makamu wa Rais.
Katika nafasi za wajumbe wa Kamati ya Utendaji, jumla ya wagombea 16 wamevuka hatua ya awali ya mchujo. Waliopitishwa ni Julius Koyi, Saady Khimji, Fredy Mahembe, Munir Seleman, Mshindo Msolla, Issa Mangungu, Mustapha Himba, Alexander Ngai, Gerald Kihinga, Yanga Makaga, Fahd Afif, Rodgers i Gumbo, Seif Gulamali, Mohamed Mwenda, Mzee Yussuf na Prisca Kishamba.Kamati ya Uchaguzi imeeleza kuwa huu ni mchujo wa awali, hivyo wagombea wote waliopitishwa wanapaswa kufika kwenye usaili wakiwa na nyaraka zao halisi kwa ajili ya kuthibitisha sifa zinazotakiwa kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya Katiba ya Klabu ya Michezo ya Yanga ya mwaka 2021 pamoja na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) za mwaka 2021.
Hatua hiyo inaweka msingi wa kuelekea uchaguzi wa viongozi wa Yanga, ambapo wanachama wa klabu hiyo watapata nafasi ya kuchagua viongozi watakaoisimamia katika kipindi kijacho.




