olise aikaribia rekodi ya Pelé kombe la dunia

Michael Olise anaendelea kuwa mmoja wa wachezaji wanaovutia zaidi katika Kombe la Dunia 2026 kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutengeneza mabao.
Kiungo huyo wa Ufaransa tayari ametoa pasi nne za mabao ndani ya mechi nne za Kombe la Dunia, jambo lililomfanya kuwa kinara wa orodha ya watoa pasi za mabao kwenye mashindano hayo hadi sasa.
Olise sasa amebakiwa na pasi moja tu kusawazisha rekodi ya gwiji wa Brazil, Pelé, ambaye ndiye anayeshikilia rekodi ya pasi nyingi zaidi za mabao katika Kombe la Dunia moja akiwa na sita.
Mbali na kiwango chake kwenye World Cup, Olise pia anaendelea kuwa na msimu wa kipekee. Kufikia sasa ametoa jumla ya pasi 31 za mabao akiwa na klabu na timu ya taifa, rekodi inayomweka miongoni mwa wachezaji bora duniani katika kutengeneza nafasi za kufunga.
Akiwa bado anaendelea na mashindano, nyota huyo wa Ufaransa ana nafasi kubwa ya kuivunja rekodi ya Pelé ikiwa ataendelea na kiwango chake katika hatua za mtoano.




