Ligi Kuu

Abuya: Tutaendelea kupambana kutimiza malengo yetu

ARUSHA: MCHEZAJI wa Yanga, Duke Abuya, amesema ushindi na tuzo ya mchezaji bora aliyopata katika mchezo dhidi ya Fountain Gate ni matokeo ya ushirikiano wa timu nzima na sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki.

Akizungumza baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate kwenye Sheikh Amri Abeid Stadium mkoani Arusha, Abuya amewashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi pamoja na wachezaji wenzake kwa mchango wao.

“Nashukuru mashabiki kwa kuja kwa wingi na pia wachezaji wenzangu kwa sababu bila wao nisingepata tuzo hii,” amesema Abuya.

Kiungo huyo amesisitiza kuwa yeye na wenzake wataendelea kupambana katika michezo iliyosalia ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya na kutimiza malengo waliyojiwekea msimu huu.

“Nawaahidi mashabiki kuwa tutaendelea kupambana kupigania pointi tatu katika michezo yetu iliyobaki ili kuhakikisha tunapata ushindi na kutimiza malengo tuliyojiwekea,” ameongeza.

Baada ya mchezo huo Yanga wameanza safari ya kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam FC.

Related Articles

Back to top button