Muziki

Chief Godlove amtambulisha msanii mpya

 DAR ES SALAAM:MENEJA na mdau maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Godlove Mwakibete ‘Chief Godlove’, amemtabulisha rasmi msanii wake mpya anayefahamika kwa jina la Agness Silvester Samson kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Chief Godlove amesema kuwa ana imani kubwa na uwezo wa msanii huyo mpya kiasi cha kutoa ahadi nzito kwamba endapo hatofanikiwa kufanya vizuri kwenye muziki, yupo tayari kugawa mali zake kwa maskini.

Agness anatajwa kuja kama mbadala wa Pipi Jojo ambaye kwa sasa anafanya kazi zake chini ya usimamizi wa Nandy.

Baada ya kutambulishwa kwake, mashabiki wengi mitandaoni wameanza kujadili zaidi kuhusu muonekano na uzuri wa msanii huyo mpya, huku baadhi wakisema ana mvuto mkubwa unaoweza kumpa nafasi ya kutikisa game la wasanii wa kike Bongo.

Swali kubwa limebaki kwa mashabiki: Je, Agness anaweza kuwazidi kwa uzuri na mvuto wasanii wengine wa kike wa Bongo Fleva?

Maoni yanaendelea kugawanyika mitandaoni huku wengi wakisubiri kuona kipaji chake pamoja na muziki atakaokuja nao rasmi.

Related Articles

Back to top button