Afrika yampagawisha federal
Rapa anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Hip hop kutoka Marekani, Federal Da General, amewaonjesha mashabiki ladha ya albamu yake mpya kwa kuachia nyimbo tano: “Your Body,” “Dropicana Assa Anna,” “Pop Yo Cherry,” “I Gotta It,” na “Love My Chicken.”
Federal ameachia nyimbo hizo kwenye mitandao kadhaa ya kusikiliza na kupakua nyimbo, na ndani ya muda mfupi mashabiki wamemiminika kwenye mtandao wa Spotify na YouTube kuzisikiliza.
Akizungumzia wimbo “Your Body,” Federal amesema aina ya rap anayoifanya imefanikiwa kupenya zaidi Afrika kuliko Marekani, na hivyo anaamini mashabiki wake wengi wapo Afrika Mashariki.
“Hii imenishangaza, ninapendwa sana Afrika. Nina mashabiki wengi Afrika Mashariki, unaweza kuona kwenye nyimbo nilizotoa zinafuatiliwa zaidi kuliko hapa Marekani,” amesema Federal.
Federal Da General anaendelea kuvutia mashabiki wapya kwa kutoa muziki wenye ladha tofauti na ujumbe mzito, na anatarajiwa kuwa mmoja wa wasanii wakubwa wa Hip hop duniani.