Ligi Daraja La Kwanza

Tanzania yajiandaa kushiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola

DODOMA:SERIKALI inaendelea kuimarisha maandalizi ya wanamichezo wake watakaoiwakilisha nchi katika Michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Glasgow, Scotland mwaka 2026, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuinua ushindani wa kimataifa wa michezo ya Tanzania.

Akizungumza bungeni, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Tanzania itatuma jumla ya wanamichezo 11 kushiriki katika michezo hiyo mikubwa ya kimataifa.

Wanamichezo hao watashiriki katika michezo ya riadha, ngumi, judo na kuogelea, huku maandalizi yao yakiendelea katika kambi mbalimbali nchini na nje ya nchi kulingana na mahitaji ya kila mchezo.

Kwa mujibu wa Makonda, kambi ya riadha imewekwa Arusha, kuogelea iko Afrika Kusini, wakati judo inaendelea Ukonga jijini Dar es Salaam, hatua inayolenga kuhakikisha wanamichezo wanapata maandalizi bora na ya kitaalamu.

Makonda amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Tanzania inaboresha zaidi matokeo yake ya kimataifa, ikikumbushia mafanikio ya awali ambapo wanamichezo walifanikiwa kutwaa medali tatu katika michezo iliyopita.

Amesema kupitia uwekezaji katika michezo na maandalizi ya kitaalamu, Serikali inalenga kuongeza idadi ya medali na kuimarisha ushindani wa Tanzania katika jukwaa la kimataifa.

Related Articles

Back to top button