KMC: Tutafufukia kwa Singida BS

SINGIDA: IKIWA imetoka kupoteza michezo minne mfululizo, Klabu ya KMC FC imesema ipo tayari kupambana na kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika mchezo unaokuja dhidi ya Singida katika Ligi Kuu ya Tanzania kesho.
Ofisa Habari wa KMC, Khalid Chukuchuku, amesema:“Tunataka kufufukia kwa Singida, kupambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na inawezekana,”
“Huu ni mchezo mgumu ambao kila mtu anafahamu. Hata KMC ikiwa inashika mkia, Singida haijawahi kuwa mchezo rahisi kwetu. Tumekuwa tukifungana nao katika mechi zilizopita. Hivyo, tunauendelea kwa tahadhari.”
KMC bado inashika mkia ikiwa imecheza michezo 17, kushinda miwili, sare mbili na kupoteza jumla 13 na pointi nane.
Mara ya mwisho ilishinda mchezo dhidi ya Mashujaa bao 1-0 ilikuwa Februari mwaka huu.
Msemaji wa Singida Hussein Masanza amesema timu imejipanga vizuri kubakisha pointi tatu kwenye Uwanja wao wa nyumbani.




